*KUENDELEZA UJENZI WA RELI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA (STANDARD GAUGE RAILWAY – SGR) KATIKA MAENEO YALIYOBAKI PAMOJA NA UNUNUZI WA VITENDEA KAZI (VICHA NA MABEHEWA) AMBAPO JUMLA YA SHILINGI TRILIONI 1.511 ZIMETENGA
*KUENDELEA KUBORESHA NA KUIMARISHA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATCL) KWA KUNUNUA NDEGE TATU (3), VIPURI, INJINI NA KUKARABATI MIUNDOMBINU WEZESHI. SHILINGI BILIONI 324.5 ZIMETENGWA
*UJENZI WA MELI MPYA YA ABIRIA 600 NA MIZIGO TANI 400 SHILINGI BILIONI 25, UJENZI NA UKARABATI WA VIWANJA VYA NDEGE AMBAPO SHILINGI BILIONI 108.71 ZIMETENGA
Na MWANDISHI WETU
-DODOMA
WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Akiwasilisha Bajeti ya wizara hiyo leo Mei 6, 2024 bungeni Jijini Dodoma, Profesa Mbarawa ameliomba Bunge kupitisha kiasi cha Shilingi trilioni 2.7, ili kuhakikisha utekelezaji wa Mpango kwa mwaka 2024/25, Wizara imepanga kutekeleza vipaumbele katika maeneo mbalimbali, ikiwamo utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea ambayo ni kuendeleza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway – SGR) katika maeneo yaliyobaki pamoja na ununuzi wa vitendea kazi (vicha na mabehewa) ambapo jumla ya Shilingi trilioni 1.511 zimetengwa.
“Kufufua Reli ya MGR kipande cha Kilosa – Kidatu Kilomita 108 ambapo kimetengwa kiasi cha Shilingi bilioni 1. Ukarabati wa Reli iliyopo katika ya MGR Shilingi bilioni 312.03 zimetengwa. Kuendelea kuboresha na kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege tatu, vipuri, injini na kukarabati miundombinu wezeshi. Shilingi bilioni 324.5 zimetengwa.
“Ujenzi na Ukarabati wa Meli katika Maziwa Makuu, ambapo jumla ya Shilingi bilioni 190.00 zimetengwa, ikiwamo ujenzi wa Meli Ziwa Tanganyika, ujenzi wa meli mpya ya abiria 600 na mizigo tani 400 Shilingi bilioni 25, na ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 Shilingi bilioni 35,” amesema Prof. Mbarawa
Pamoja na hali hiyo alisema kuwa katika bajeti hiyo wanatarajiwa kujenga kiwanda cha kujengea Meli chenye uwezo wa kubeba meli zenye uzito wa tani 5,000 Shilingi bilioni 30.
“Ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 Shilingi bilioni 20, ukarabati katika Ziwa Tanganyika, ukarabati wa meli ya MV Liemba Shilingi bilioni 5, ukarabati wa meli ya mafuta ya MT Sangara Shilingi bilioni 1.5 pamoja na ukarabati wa meli ya MV Mwongozo Shilingi milioni 300.
“Ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya Ndege ambapo Shilingi bilioni 108.71 zimetenga; ujenzi wa Kiwanja cha Arusha Shilingi bilioni 5.08, ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Lindi Shilingi bilioni 13 pamoja na ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Moshi Shilingi bilioni 5,” amesema
Licha hilo Mbarawa, amesema kuwa utafanyika ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida Shilingi bilioni pamoja na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Kiwanja cha Ndege cha Njombe kwa Daraja 4E. Shilingi milioni 692.
Amesema upembuzi yakinifu na usanifu wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimataifa cha Serengeti Shilingi bilioni 1, usanifu wa kina wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya TAA Shilingi milioni 400.
Pamoja na hilo alisema kuwa ujenzi wa Kiwanja cha Mwanza Shilingi bilioni 15 na ujenzi wa Kiwanja cha Bukoba Shilingi bilioni 3.48.
“Ujenzi wa Kiwanja cha Mtwara Shilingi bilioni 7.3, ukarabati wa kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro Shilingi bilioni 50, uboreshaji na Upanuzi wa Jengo la Pili la Abiria JNIA Shilingi bilioni 6.08 na kukarabati na kuboresha Reli ya TAZARA ambapo Shilingi bilioni 13.69 zimetengwa,” amesema
Licha ya hilo katika bajeti hiyo kipaumbele kingine ni kuendelea na ununuzi wa rada na vifaa vya hali ya hewa ambapo Shilingi bilioni 15.00 zimetengwa pamoja na kuendelea kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na bandari nyingine zikiwemo zilizopo katika Maziwa Makuu kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ya TPA.
Kwa upande wa maboresho Ziwa Tanganyika, Waziri Mbarawa amesema kuwa uboreshaji wa Bandari ya Kigoma kwa kujenga barabara za kiungo, Cargo Shed, Passenger Wharf and Lounge, kuendelea na ujenzi wa jengo la abiria (Passenger Lounge); na kuendelea na ujenzi wa Passenger Lounge na ukuta wa mizigo wa Lighter Quay katika Bandari ya Kibirizi na gati la Bandari ya Ujiji.
TRENI SGR
Amesema wizara yake itaanza uendeshaji wa treni ya SGR kwa kipande cha Dar es Salaam – Dodoma ambapo kwa sasa Wizara kupitia TRC inaendelea na majaribio ya miundombinu ya reli kwa ajili ya kuanza utoaji wa huduma hiyo rasmi ifikapo Julai mwaka huu.
Mbali na hilo amesema kipaumbe kingine ni kuanza kutoa mafunzo ya urubani katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa lengo la kupunguza gharama za kusomesha marubani nje ya nchi; na
“Kununua Boti ya Matibabu (Ambulance Boat) kwa ajili ya utafutaji na uokoaji katika Ziwa Victoria pale ajali zinapotokea ndani ya Ziwa hilo na kuendelea kutekeleza Mkakati wa upatikanaji wa Fedha za kigeni ambapo kwa mwaka 2024/25 pekee Wizara inatarajiwa kukusanya jumla ya Dola za Marekani milioni 762.41, sawa na takriban Shilingi trilioni 1.94.