Home KITAIFA KITITA CHA NHIF KUBORESHA ZAIDI HUDUMA

KITITA CHA NHIF KUBORESHA ZAIDI HUDUMA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema kuwa katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Wizara imeidhinisha matumizi ya kitita kipya cha mafao cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya cha mwaka 2023.

Amesema kitita hicho kimeoanishwa na orodha muhimu ya Dawa (NEMLIT) pamoja na Mwongozo wa Tiba wa Taifa (STG).

Hayo amesema leo bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akiwasilisha Bajeti ya wizara yake kwa Mwa wa Fedha 2024/25, ambapo alisema kuwa kikita hicho kitaboresha upatikanaji wa huduma bora za kibingwa na ubingwa bobezi karibu na wanachama.

“Aidha, kitita hiki kimezingatia maendeleo ya teknolojia ya tiba, hali halisi ya bei katika soko na uwezo wa Mfuko kugharamia huduma hizo huku ukiendelea kuwa endelevu kwa kuzingatia ushauri wa Taarifa ya mapendekezo ya Tathmini ya Uhai na uendelevu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 June 2021,” alisema Ummy

Pamoja na hali hiyo alisema kuwa mambo makubwa yaliyofanyiwa maboresho katika kitita cha mafao cha mwaka 2023 ni pamoja na kuongezeka kwa dawa mpya 254 zenye ufanisi ambazo awali wanachama walilazimika kutoa fedha taslimu kwa kuwa hazikuwa sehemu ya Kitita cha mwaka 2016.

“Dawa 178 ambazo hazikuwa kwenye Orodha ya Dawa Muhimu ya Taifa (NEMLIT) zimeongezwa baada ya Wizara kufanya mapitio ya NEMLIT na kutoa nyongeza (addendum) na hivyo kujumuishwa katika kitita cha NHIF cha mwaka 2023.

“Kuwaepusha wanachama kuendelea kutumia dawa zisizo na matokeo chanya hivyo kuwaepusha na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na usugu wa dawa husika; ü Kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa bobezi karibu na wananchi kuanzia Hospitali za ngazi mkoa na Kanda, kuondoa usumbufu wa kukosa baadhi ya dawa na huduma nyingine.

“…huduma hizo ni pamoja na matibabu ya saratani, upasuaji wa mifupa, upasuaji wa moyo ambazo awali zilikuwa zinatolewa katika Hospitali za ngazi ya Taifa tu pamoja na kuweka usawa wa ada ya usajili na kumuona madaktari wenye elimu na taaluma zinazofanana kwa wanufaika wa NHIF. Mathalani, kwa kitita kipya Daktari Bingwa katika ngazi ya Rufaa Mkoa ada imeongezeka kutoka Shilingi 15,000 hadi Shilingi 25,000 ambapo ni sawa na ada ya kumuona Daktari aliyeko ngazi ya Kanda na Taifa. Hatua hii itavutia madaktari bingwa kufanya kazi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa hususan ya pembezoni,” alisema Waziri Ummy

 Akizungumzia kuhusu ada ya usajili na kumuona daktari kwa wanufaika wa NHIF kwa ngazi ya Wilaya alisema  imeongezeka kutoka Shilingi 5,000 hadi Shilingi 7,000,  kwa ngazi ya Kituo cha Afya ada imeongezeka kutoka Shilingi 2,000 hadi Shilingi 7,000 na kwa ngazi ya Zahanati ada imeongezeka kutoka Shilingi 1,000 hadi Shilingi 3,000.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa hatua hiyo itaongeza mapato katika vituo na motisha kwa watumishi wa Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya na hivyo kuvutia Madaktari kufanya kazi katika vituo hivi; 68.

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kuwa huduma za afya zinabadilika mara kwa mara kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia na hali halisi ya soko, ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza na kukua kwa Sekta ya Afya 31 ya umma na binafsi, NHIF itafanya mapitio ya kitita cha mafao yake kila baada ya miaka miwili.

Aidha, alisea kuwa Serikali inakusudia kuanzisha Chombo cha Kitaifa cha Udhibiti wa Bei za Huduma za Afya katika ngazi zote nchini kama inavyofanyika kwenye udhibiti wa gharama za maji, umeme na mafuta.

“Lengo ni kudhibiti ukuaji holela wa gharama za afya kwa wananchi hususan wasio na bima ya afya,” alisema Ummy

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here