Home KITAIFA UMMY ALIOMBA BUNGE TRILIONI 1.31 BAJETI WIZARA YA AFYA

UMMY ALIOMBA BUNGE TRILIONI 1.31 BAJETI WIZARA YA AFYA

Google search engine
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

WIZARA ya Afya Ummy Mwalimu ameomba Bunge kuidhinisha mpango wa bajeti ya mapato na matumizi wa Shilingi trilioni 1.31 kwa mwaka wa fedha 2024/25 ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za kinga na kibingwa nchini.

Akiwasilisha Hotuba Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 13, Waziri Ummy amebainisha vipaumbele 10 ambavyo vvinahusisha kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa, kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya katika vituo vya afya kwa ngazi zote, kuimarisha huduma za afya za uzazi, mama na mtoto kuimarisha upatikanaji wa wataalam katika sekta ya afya katika fani za kati, ubingwa na ubingwa bobezi.

Vilevile, Waziri Ummy amesema bajeti yake inalenga kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi nchini kusimamia afua za Tiba Asili na Tiba Mbadala, kuimarisha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa ya mlipuko na huduma za afya za dharura. “Pia tunakusudia kuimarisha huduma za afya ya akili ambapo kiasi kilichotengwa kwenye eneo hilo ni Sh 5,618,528,988,” amesema Waziri Ummy.

Ameongeza kuwa, Wizara inakusudia kuimarisha huduma za utengamao na tiba shufaa hususani kwa watoto, wazee na wenye ulemavu pamoja na kusimamia tafsiri na matumizi ya matokeo ya tafiti mbalimbali za afya na kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here