Home BIASHARA BENKI YA TCB YATENGENEZA FAIDA YA SHILINGI  BILIONI 19.27

BENKI YA TCB YATENGENEZA FAIDA YA SHILINGI  BILIONI 19.27

Google search engine
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo, akiwasilisha taarifa ya benki hiyo ya mwaka 2023 katika Mkutano Mkuu wa 32 wa wanahisa wa benki hiyo, uliofanyika leo Juni 18, 2024, Jijini Dar es Salaam

Na MWANDISHI WETU

– DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo amesema kuwa Benki hiyo imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato ya jumla ya Shilingi bilioni 19.27 sawa na asilimia 11.19 hadi kufika bilioni 19. 21, kwa mwaka 2023, ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo mapato yalikuwa bilioni 172.83 sawa na asilimia 1.72.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya benki hiyo ya mwaka 2023 katika Mkutano Mkuu wa 32 wa wanahisa wa benki hiyo.

Amesema kuwa ongezeko hilo lilichangia asilimia 79.61 ya mapato yote ya benki, huku kiasi kilichobaki kikipatikana kutoka katika kamisheni, ada mbalimbali na shughuli nyingine zilizofanywa na benki.

Aidha, ameongeza kuwa taasisi hiyo ina dhamira ya dhati ya kudumisha ufanisi na kumridhisha mteja sambamba na kusikiliza na kuelewa mahitaji ya wateja wake .

Katika mkutano huo Mihayo amefafanua kwa undani mafanikio waliyoyapata mwaka 2023,  ambapo amesema kuwa mali za benki hiyo, ziliongezeka kutoka Shilingi trilioni 1.285 mwishoni mwa mwaka hadi kufikia tririon 1.389 mwishoni mwa mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 8.1 ikiwa ni sawa na Shilingi bilioni 103. 9.

“Jumla ya mikopo yote iliongezeka kwa Shilingi bilioni 73.1 kutoka bilioni 838 mwishoni mwa mwaka 2022 mpaka kufika bilioni 911.2 mnamo Desemba 31, 2023 ikionyesha ongezeko la amana za wateja ambazo ziliongezeka kwa asilimia 12.01 kutoka trillion moja mwishoni mwa mwaka 2022, hadi kufika trilioni 1.12 mwishoni mwa mwaka 2023,” amesema Mihayo.

Pia amesema, kupitia usimamizi wa kimkakati wa uwekezaji wake, amana za Benki ya TCB katika benki nyingine zilishuka kwa Shilingi bilioni 55.3  ambayoni sawa na asilimia 33.32, huku amana za Serikali zikiongezeka kwa Shilingi bilioni 44.1 sawa na asilimia 42.64, fedha tasilimu, ambapo salio katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) liliongezeka kwa Shilingi bilioni 47 sawa na asilimia 41.26.

Mbali na hayo, Mihayo amesema benki hiyo imeboresha mifumo yake ya kibenki kwa kuanzisha mradi unaowawezesha watumiaji wa mtandao wa Tigo kutoa hela zao katika mashine za ATM za benki hiyo.

Aidha, amesema kuwa majaribio ya mashine za ATM zinazowawezesha wateja kuweka fedha zao tayari yamefanyika, ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu.

“Tutaendelea kuhakikisha tunawawezesha kupata suluhisho la kifedha katika mahitaji yao mbalimbali, ili kuchangia katika mafanikio ya Watanzania kama ambavyo dhamira yetu ya kuwezesha ukuaji wa kiuchumi wa watu wetu inavyoeleza,” amesema

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here