Home KITAIFA KEYSHA AANGUA KILIO BUNGENI MAUAJI YA MTOTO MWENYE UALBINO

KEYSHA AANGUA KILIO BUNGENI MAUAJI YA MTOTO MWENYE UALBINO

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Dodoma, Khadija Taya maarufu Keysha amejikuta akiangua kilio bungeni wakati akiliomba Bunge kujadili matukio ya watoto wawili wenye ualbino waliofanyiwa vitendo vya ukatili kwa kukatwa viungo vyao vya mwili jambo lililopelekea kifo cha mmoja wa watoto hao.

Akibubujikwa na mchozi wakati akiliomba Bunge kuahirisha shughuli zake na kujadili suaa la watoto hao Keysha alisema mnamo Mei 4, mwaka huu huko wilayani Geita, Mkoa wa Geita, mtoto aliyefahamika kwa jina la Julius Kazungu (10) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kichwani na eneo la mkononi kwake na kumsababishia maumivu makali.

Aidha, Mei 30, 2024 mtoto anayeitwa Assimmwe Novas (2) anadaiwa kuibwa na watu wasiojulikana ambao walivamia nyumbani kwa mama yake na kumchukua mtoto huyo na kwenda naye sehemu pasipojulikana licha ya Serikali kufanya kazi kubwa ya kumtafuta, hata hivyo mtoto huyo alikutwa jana (Juni 17) akiwa akiwa ameshakufa na mwili wake ukiwa umekatwa baadhi ya viungo.

“Mheshimiwa Naibu Spika hapa ninapozungumza, watu wenye ualbino hawana amani, hawana raha wanaamini kwamba karibia na uchaguzi maisha yao yanakuwa hatarini, na sisi ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakwenda kwenye uchaguzi,

“Hivyo Mheshimiwa Naibu Spika kwa maumivu waliyonayo watu wenye ualbino, kwa maumivu ya wazazi ambao watoto wao wamejeruhiwa, mtoto wa miwili ameondolewa viungo vyak. Mheshimiwa Naibu Spika naomba Bunge lako liahirishe shughuli zake tujadili namna gani nzuri ya kuwalinda watu wenye ualbino na watoto wetu,

“Niiombe Serikali kuleta sheria kali ambazo zitaweza kuondoa au kuonyesha mfano kwa wengine kutokufanya vitendo hivi. Naomba sana Bunge na kiti chako kikubali na liridhie, lakini naomba kutoa hoja wenzangu wanisaidie kujadili jambo hili,” alisema Keysha.

Pamoja na hali hiyo ameitaka Serikali kuweka sheria kali kukomesha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino kufatia tukio la mtoto mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa Geita kukatwa viungo na kusababisha kifo chake.

 “Mheshimiwa Naibu Spika hapa ninapozungumza, watu wenye ualbino hawana amani, hawana raha wanaamini kwamba karibia na uchaguzi maisha yao yanakuwa hatarini, na sisi ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakwenda kwenye uchaguzi,

“Hivyo Mheshimiwa Naibu Spika kwa maumivu waliyonayo watu wenye ualbino, kwa maumivu ya wazazi ambao watoto wao wamejeruhiwa, mtoto wa miwili ameondolewa viungo vyake. Mheshimiwa Naibu Spika naomba Bunge lako liahirishe shughuli zake tujadili namna gani nzuri ya kuwalinda watu wenye ualbino na watoto wetu.

“Lakini pia tuitake Serikali kuleta sheria kali ambazo zitaweza kuondoa au kuonyesha mfano kwa wengine kutokufanya vitendo hivi. Naomba sana Bunge na kiti chako kikubali na liridhie, lakini naomba kutoa hoja wenzangu wanisaidie kujadili jambo hili,” alisema Keysha.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here