Home MAKALA UZIO WA PILIPILI UNAVYOSAIDIA WAKAZI TUNDURU KULINDA MAZAO YAO DHIDI YA TEMBO

UZIO WA PILIPILI UNAVYOSAIDIA WAKAZI TUNDURU KULINDA MAZAO YAO DHIDI YA TEMBO

Google search engine
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbati, Baslom Mnkondya, akieleza kwa waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) kuhusu hali migongano kati ya Binadamu na Wanyamapori wakiwamo Tembo katika kijiji hicho

Na BAKARI KIMWANGA

-ALIYEKUWA TUNDURU

Katika jamii nyingi vijijini kama kijiji cha Mbati katika kata ya Mbati, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma ambacho kipo karibu na shoroba ya Wanyama pori ya Selous-Niassa inayounganisha Hifadhi ya Selous na Hifadhi ya Niassa ya Msumbiji.

Wakazi wa Mbati wamekuwa wakipambana na wanyama wakubwa kwa miaka mingi kwani wanyama pori wanatembelea vijiji karibu na njia za uhamiaji wa wanyama pori kutafuta chakula. Changamoto ya Migogoro ya Binadamu na Wanyamapori (HWC) si tu katika kijiji cha Mbati katika Wilaya ya Tunduru, bali katika nchi nzima na bara zima.

Kwa mujibu wa taarifa za mamlaka, tembo wamekuwa wakivamia vijiji katika Kata ya Mbati ambao wamekuwa wakilima mazao mengi ya chakula na biashara, jambo ambalo limekuwa likiwavutia wanyama pori kula mazao yaliyokomaa.

Mazao yanayolimwa zaidi ni pamoja na mpunga, maharage, mbaazi, mahindi, korosho na karanga.

“Hivi karibuni, tembo walivamia na kuharibu ekari mbili za mashamba yangu ya karanga na mahindi. Tatizo linazidi kuwa kubwa kila siku; matukio mengi hutokea kati ya Januari na Julai kila mwaka,” alisema Hamida Said, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruvuma.

Mkazi wa Kitogoji cha Mbati ya Leo, Mohamed Magawa akionyesha uzio wa pilipili uliowasaodoa kupata mazao katika shamba lao la pamoja ambao walipata utalaamu huo kutoka GIZ

Mohamed Magawa ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mbati, Kitongoji cha Mbati ya Leo, anasema changamoto hiyo inaleta tishio kwa watu na mashamba pia.

Anasema hakuna wakati maalum kwa uvamizi usiotarajiwa kwani tembo wanaweza kuingia mashambani asubuhi, mchana na usiku.

Magawa alitoa pongezi kwa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia Serikali ya Ujerumani (BMZ) kwa kuanzisha mradi wa Kupunguza Migogoro ya Binadamu na Wanyamapori nchini Tanzania ili kuwasaidia kukabiliana na uvamizi wa tembo katika mashamba yao.

Anasema kabla ya hatua hizo walikuwa wanapitia usiku kucha huku wakipigwa na baridi ili kulinda mazao y shambani ila kuwa na zana yoyote ya kujilinda.

Mradi huo unatekelezwa katika ukanda wa Ruvuma ukiwalenga watu wa vijijini katika vijiji vilivyopo kusini mwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na Pori la Akiba la Selous katika Wilaya za Liwale (Lindi), Namtumbo na Tunduru katika Mkoa wa Ruvuma.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mbati ya Leo, wakifurahia ujio wa wanahabari katika kijiji chao ili kusikiliza hali ya mgongano wa binadamu na Wanyamapori, ambapo walipewa nakala za magazeti ya Kasuku ili waweze kupata elimu zaidi

“Tunashukuru GIZ kwa kutusaidia kujenga uzio wa pilipili kuwalinda mashamba yetu. Uzio huo umethibitisha ufanisi kwani mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa tumeweza kupata mavuno mengi. Tunajaza chupa za maji na unga wa pilipili, viungo ambavyo tembo wanachukia sana harufu yake na kuziweka katika uzio wetu kwa kutumia kamba ya za mkonge,” anasema

Anasema awali walikuwa wakitumia sauti kama njia ya kuwafukuza tembo pindi wanapoingia kenye mashamba yao au hata kupiga kelele, kupiga madumu kama njia ya kuswaga wanyamapori ho ili waondoke kwenye mashamba yao.

Yassin Mkwanda ni mmoja wa Askari wa Uhifadhi wa Kijiji (VGS), anasema hivi karibuni walikuwa vijana watatu abao wametoka katika Kijiji cha Mbati ambao wamehitimu hivi msfunzo kutoka Kituo cha Mafunzo ya Uhifadhi ya Msingi ya Jamii (CBCTC) – Likuyu Sekamaganga katika Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma.

Anasema anajipanga kutmia maarifa aliyopata kwa kutwafundisha pia wakazi wenzake ili nao waweze njia sahihi za k kuwafukuza tembo wanapoingia kwenye mashamba yao na makazi.

“Ujenzi wa uzio wa pilipili umepunguza changamoto kwa asilimia 85, nmepanga kuwaelimisha wakazi juu ya umuhimu wa uzio, lakini pia, wasiende mashambani mapema asubuhi ili kuepuka kukutana na tembo,” anasema Mkwanda na kutoa wito kwa serikali ya kijiji na wafadhili kuwapa vifaa wanavyohitaji.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Mbati, Baslom Mnkondya anasema kijiji kilichoanzishwa mwaka 1972 na kusajiliwa rasmi mwaka 1974 kina idadi ya watu 3,575, kati yao, 1,759 ni wanaume na 1,808 ni wanawake kulingana na takwimu za sensa ya makazi na idadi ya watu ya mwaka 2022.

Mnkondya anabainisha kuwa HWC ni tatizo kubwa katika eneo hilo ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, kati ya watu 85 na 100 walikuwa na mazao yao kuliwa na mashamba yao kuharibiwa na tembo.

Anasema mwaka huu zaidi ya 150 wameharibiwa na tatizo hilo ni kubwa zaidi katika maeneo ya Ruvuma, Mwinyi, Mbati ya Leo, Muungano, Mandeka na Nyasa.

Naye Diwani wa Kata ya Mbati, Rashid Salehe ameiomba serikali kuajiri maafisa wa wanyamapori zaidi kwani idadi yao ni ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa wilaya.

“Tuna maafisa wa wanyamapori saba tu katika wilaya yetu; tunashukuru GIZ kwa kufadhili VGS watatu kupitia mafunzo ya kukabiliana na HWC,” anasema Swalehe akisisitiza umuhimu wa elimu kwa wakazi ili wawasaidie juhudi za kupanua na kuachilia njia za wanyama pori, ili wanyama waweze kutembea kwa uhuru zaidi bila kukutana na binadamu.

Timu ya waandishi wa habari ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo, ikitembelea mashamba ya wananchi katika Kitongoji cha Mbati ya Leo Wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma ili kuona hali ya mgongano wa Binadamu na Wanyamapori

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Bosco Mwingira, anasema tatizo hilo ni kubwa zaidi katika eneo hilo kwani linapakana na Hifadhi ya Niassa ya Msumbiji ambapo tembo wamekuwa wakihamahama kutoka upande mmoja hadi mwingine.

Mwingira anabainisha kuwa matukio ya uvamizi wa mashamba yanazidi kuongezeka wakati mazao mengi yanapokuwa yanakomaa, hivyo kuvutia wanyama hao.

Anasema wilaya yenye vijiji 157 na kata 39 inakabiliwa na uhaba wa maafisa wa wanyamapori.

“Tunaitaka serikali kuu iteue maafisa wa wanyamapori zaidi kwa wilaya yetu; pia tunawaomba wafadhili na mashirika mengine kutusaidia na vifaa ili kuwezesha VGS kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” anaongeza, akibainisha kuwa wilaya inatenga Shilingi milioni 15  kila mwaka kwa ununuzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kuwatisha na kuwafukuza tembo.

Anasema ukusanyaji wa mapato ya wilaya sasa umepanda hadi Shilingi bilioni 5.6 kutoka Shilingi bilioni  4.8 ya awali ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo zinaelekezwa kwenye utoaji wa huduma za kijamii.

Shafii Msuya ni Mshauri wa Kiufundi, Kupunguza Migogoro ya Binadamu na Wanyamapori katika Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, anasema wanafanya kazi katika vijiji 30 katika eneo hilo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here