Home KITAIFA NMB YAPIGA JEKI HOSPITALI DKT. JAKAYA KIKWETE, SHULE ZA MSINGI

NMB YAPIGA JEKI HOSPITALI DKT. JAKAYA KIKWETE, SHULE ZA MSINGI

Google search engine

NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhimarisha huduma mbalimbali za kijamii, Benki ya NMB imetoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh Milioni 44 katika sekta ya Afya na Elimu kwenye mikoa ya Shinyanga na Dar es Salaam.

Katika sekta ya Afya Benki hiyo imetoa vifaa vya kutolea huduma za Afya vyenye thamani ya Sh Milioni 24 katika Hospitali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Hospitali ya Wilaya ya Kishapu) pamoja na Zahanati mbili za Busongo na Ng’wanhalanga zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Kwenye Sekta ya Elimu, NMB imetoa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi milioni 20 kwa ajili ya wanafunzi na walimu wa Shule za Msingi Karakata na Bangulo zilizopo Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.

Vifaa vya Afya vilivyotolewa ni vitanda vya kubebea wagonjwa vitatu, vitanda vya kujifungulia 12, vitanda vya uchunguzi sita, magodoro 14, pamoja na vitanda vya kulalia wagonjwa 14 .

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio,  alisema kuwa alisema afya na elimu ni kati ya Sekta za Kipaumbele kwa NMB, ambazo zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa cha asilimia moja ya faida ili kusaidia utatuzi wa changamoto kwenye jamii.

Afisa Tawala Mkuu Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja, akifurahi pamoja na baadhi ya wanafunzi Queen Andrea (kulia) na Halima Yusuph, baada ya kupokea zawadi ya Madawati 125, Viti na Meza zake kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Uwanja wa Ndege, Restus Assenga (wa kwanza kushoto waliosimama)  wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi milioni 20 iliyofanyika Shule ya Msingi Karakata jijini Dar es Salaam. 

“Changamoto za Afya na Elimu kwa benki yetu ni jambo la kipaumbele na hii ni kutokana na ukweli kwamba nyanja hizo ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote, ndio maana sisi hutenga asilimia moja ya faida yetu kila mwaka kusaidia sekta hizo pamoja na majanga,” alisema

Mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa, Macha alipongeza benki ya NMB kama mfano wakuigwa kwenye setka binafsi kwa jinsi inavyo unga mkono mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma kwa jamii.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mlyutu aliishukuru NMB kwa kusaidia sekta ya afya katika mkoa wa Shinyanga ikiwemo mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu.

Kwa upande wa vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya shule za msingi za jijini Dar es salaam ni pamoja na madawati 125, viti 50 na meza 50 kwa ajili ya shule zote mbili, ambavyo vilikabidhiwa na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Airport Restus Assenga.

Assenga wakati akizungumza kabla ya kukabidhi alisema kuwa changamoto za Sekta ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya NMB, ambayo hutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi ya kila mwaka, kusaidia utatuzi wake, kama inavyofanya katika afya na majanga.

“Tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kufanikisha utoaji elimu bora na bure mijini na vijijini, nasi kama wadau tunajiona tunao wajibu wa kuunga mkono hilo, ndio maana NMB hutenga asilimia moja ya faida yetu kurejesha kwa jamii,” alisema Assenga.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali Afisa Tawala Mkuu Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja alishukuru NMB kwa kutoa vifaa hivyo, huku akisisitiza walimu na wanafunzi kuhakikisha wanavitunza.

Afisa Tawala Mkuu, Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja (kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa madawati 125, viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya Shilingi milioni 20 kutoka kwa Meneja wa NMB Tawi la Airport, Restus Assenga (kulia) kwa ajili ya wanafunzi na walimu wa Shule za Msingi Karakata na Bangulo zilizopo Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam. Na Mpigapicha Wetu
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here