Home KITAIFA AMREF YAIPONGEZA NMB KUCHANGIA MILIONI 60/- UZAZI NI MAISHA ZANZIBAR

AMREF YAIPONGEZA NMB KUCHANGIA MILIONI 60/- UZAZI NI MAISHA ZANZIBAR

Google search engine
Waziri wa Afya Zanzibar, Nasoro Ahmed Mazrui (katikati), akipokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame (kulia), wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na wadau wa sekta ya afya ikiwemo NMB. Hafla hiyo ilifanyika jijini Zanzibar Juni 24, 2024. kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa. Na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Afya Zanzibar, Nasoro Ahmed Mazrui (wa pili kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame (wapili kulia), wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na wadau wa sekta ya afya ikiwemo NMB. Hafla hiyo ilifanyika jijini Zanzibar Juni 24, 2024. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Habiba Hassan Omari kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa. Na Mpiga Picha Wetu.

Na MWANDISHI WETU

-ZANZIBAR

 SHIRIKA la AMREF Health Africa – Tanzania, limeipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia vifaa tiba vya Shilingi milioni 20.17 katika mwaka wa mwisho wa Kampeni ya Uzazi Salama ijulikanayo kama Uzazi ni Maisha, hivyo kufanya mchango wa jumla wa benki hiyo kufikia Shilingi milioni  60.17 katika kipindi cha miaka mitatu tangu kampeni hiyo ianze mwaka 2022.

 Uzazi ni Maisha inaendeshwa na AMREF kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar – kupitia Wizara ya Afya, ilizinduliwa mwaka 2022 na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ikilenga kukusanya Shilingi bilioni moja ama vifaa tiba vyenye thamani hiyo kwa ajili ya kusambaza katika Vituo vya Afya 28, Zanzibar.

Kupitia Uzazi ni Maisha – kampeni iliyohusisha Matembezi, Mbio Fupi na Ndefu (Wogging – Walk-Jog-Run), imeingia katika mwaka wa tatu na mwisho, ambako imekusanya takribani pesa taslimu na vifaa tiba vya Shilingi milioni. 743.5, kati ya hizo Shilingi milioni 60 zikitolewa na Benki ya NMB pekee.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkaazi wa AMREF Health Africa – Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa, alisema kuwa bado kuna ahadi mbalimbali za jumla ya Shilingi milioni 900 kutoka kwa wadau tofauti.

 “AMREF tunaishukuru sana Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa kufanikisha makusanyo haya, na wakati tukiwaomba wadau ambao hawajatimiza ahadi zao kufanya hivyo kabla ya mwisho wa mwaka, tunaiomba tena Serikali kusaidia gharama za kuingiza nchini ‘mobile van’ 10 zilizoko jijini Nairobi, Kenya.

Waziri wa Afya Zanzibar, Nasoro Ahmed Mazrui (katikati), akikagua kitanda cha kujifungulia akina mama wajawazito mara baada ya kupokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame (wapili kulia), wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na wadau wa sekta ya afya ikiwemo NMB. Hafla hiyo ilifanyika jijini Zanzibar Juni 24, 2024. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Habiba Hassan Omari na wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dkt. Serafina Mkuwa. Na Mpiga Picha Wetu.

 “Shukrani zetu za dhati ziwafikiewatu binafsi, taasisi, mashirika, kampuni na wadau wa afya walioguswa na kampeni yetu ya kuokoa maisha ya mama na mtoto, kiasi wakakubali kuchangia pesa na vifaa tiba hivi na vingine ambayo tumeshakabidhi, vinavyoenda kusaidia huduma za uzazi kote Zanzibar,” alisema.

 Katika mahojiano maalum baada ya makabidhiano hayo, Dkt. Serafina aliipongeza na kuishukuru NMB kwa kuchangia vifaa tiba vya Shilingi milioni  20.17 vilivyotolewa katika hafla hiyo, na kufanya mchango wao wa jumla kufikia Shilingi milioni  60 baada ya awali kuchangia Shilingi milioni  40 katika mwaka wa kwanza.

 “Kipekee na kwa dhati tunapenda kuishukuru Benki ya NMB kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kampeni yote ya Uzazi ni Maisha Wogging, ni msaada muhimu unaoenda kuchangia pakubwa lengo letu la jumla la kukusanya vifaa tiba kwa ajili ya Vituo vya Afya Teule 28.

 “Tunawashukuru kwa sababu NMB imekuwa bega kwa bega sio tuna AMREF Health Africa, bali na Wizara ya Afya pia, tangu siku ya mwanzo wa kapeni hii mwaka 2022 na naamini hata sasa tunapoelekea kuhitimisha kampeni hii mwaka huu, ushirikiano wao nasi utaendelea,” alisisitiza Dkt. Serafina.

 Kwa upande wake, Meneja wa Biashara wa NMB Zanzibar, Naima Shaame, alisema vifaa tiba walivyokabidhi kwa Amref Health Afrika – Tanzania, nayo kuvikabidhi kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, ni vitanda vya kujifungulia 11, mashuka 250 na mizani ya kupimia uzito 30.

 “Katika mwaka wa kwanza wa kampeni hii, NMB tulichangia vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni  40, tukisukumwa na ukweli kwamba afya ni miongoni mwa sekta za kipaumbele kwa benki yetu na leo hii tuko hapa kukabidhi msaada wa Shilingi milioni  20.17 kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Tunawashukuru AMREF na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia Wizara ya Afya kwa ushirikiano waliotuonesha, tulivutiwa na malengo yao, na kutokana na kutambua wajibu wetu kwa jamii inayotuzunguka, tukawiwa kuchangia vifaa hivyo kwa ustawi wa afya ya kina mama Zanzibar.

 “AMREF Health walipotuomba, tuliona ni fursa ya kuendeleza Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), tukajitosa kuhakikisha mama na mtoto wanabaki salama. NMB, siri ya mafanikio yetu ni mwananchi na tunamuangalia mteja tangu akiwatumboni, tunapomtunza mama, tunalea mteja wetu wa baadaye,” alisema Naima.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here