Home KITAIFA RC MTANDA AIPONGEZA MSD KWA MAGEUZI YA UTENDAJI

RC MTANDA AIPONGEZA MSD KWA MAGEUZI YA UTENDAJI

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa ugatuzi wa madaraka kwa Kanda zake nchini, kwani uamuazi huo utasaidia na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za afya kwa wakati.

Mtanda ametoa pongezi hizo hapo jana, wakati akifunga kikao kazi baina ya MSD na Wateja wake wanaohudumiwa na  Kanda ya Mwanza ambao ni kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu na Geita.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa licha ya kuokoa muda wa manunuzi, ugatuzi huo madaraka kwa Kanda, utasaidia kupunguza mzigo wa majukumu kwa MSD Makao Makuu, na kuleta ufanisi.

Pamoja na hali hiyo pia ameipongeza Mènejimenti ya MSD kwa utaratibu wake wa kukutana na wadau na wateja wake, kujadiliana na kutatua changamoto za upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Awali akifungua kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kuwa maboresho mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bohari ili kuleta tija katika kuwahudumia Wateja wake.

“Hivi sasa MSD imewekeza nguvu katika kuboresha maeneo yake ya Uhifadhi kwa kujenga maghala ya kisasa katika Kanda zake mbalimbali ili kuongeza uwezo wa Kanda hizo kuhudumia wateja wake,” amesema Mavere

Aidha, amebainisha kuhusu mabadiliko na maboresho ya mikataba ya manunuzi hali iliyopelekea kuongezeka kwa bidhaa ghalani na uwezo wa MSD kukidhi mahitaji ya Wateja.

Amesema kuwa atika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2023/24, mapato ya bidhaa za afya yameongezeka kutoka kiasi cha Shilingi bilioni 266 na kufikia takribani Shilingi bilioni 530, sawa na ongezeko la takribani asilimia 100.

Katika hatua nyingine Mavere amegusia maboresho ya eneo la huduma kwa wateja kwa kuimarisha mawasiliano na mahusiano na wateja, hivyo kuondoa malalamiko na misuguano isiyo ya lazima.

Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza, Egidius Rwezaura amewashukuru wadau hao kwa kuitikia wito wa kuhudhuria kikao hicho, na kuwataka kuendelea kushirikiana ili kutatua kwa pamoja changamoto za upatikanaji wa bidhaa za afya

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here