Home KITAIFA DC SIMA AWATAKA WATEJA MSD KULIPA MADENI YAO

DC SIMA AWATAKA WATEJA MSD KULIPA MADENI YAO

Google search engine
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa MSD kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa. mkutan huo ulifuguliwa mjini Bukoba
Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD, Victor Sungusia

Na MWANDISHI WETU

-KAGERA

WADAU wa afya kwenye mikoa ya Kagera na Geita, wameaswa  kulipa madeni wanayodaiwa na Bohari ya Dawa (MSD), kama lengo la kuleta ufanisi kwa taasisi hiyo.

Madeni hayo yanayokaridiwa kufikia Shilingi bilioni 6.5, ikiwa yatalipwa na wateja hao yataiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa weledi katika kununua, kutunza na kusambaza bidhaa za afya sambamba na kulipa washitiri wanaofanya nao biashara na kuufanya mnyororo wa upatikanaji wa bidhaa za afya nchini kuwa endelevu.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa MSD na wateja wake kutoka mikoa ya Kagera na Geita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

DC Sima, amesema uwepo wa limbikizo makubwa ya madeni ambao yanadaiwa na MSD kwenye vituo vya kutolea huduma za afya yanaathiri kwa kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa taasisi hiyo na hata kukwamisha uwezo wake kutoa huduma kutokana na kuzidiwa na mahitaji yanayasababishwa na uhaba wa fedha.

“Wadau endeleeni kushirikiana na MSD kama njia ya kuboresha uhusiano na mawasiliano baina yetu ikiwamo kwa pamoja muweze kujadiliana ili kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili na kuathiri mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwenye maeneno yetu ya kutolea huduma hasa bidhaa za afya,” amesema DC Sima

Awali akizungumza kwenye kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD, Victor Sungusia, amesema MSD imefanya maboresho huduma zake kwa kiasi kikubwa,  ikiwemo upatikanaji wa bidhaa za afya.

“Hivi sasa uwezo MSD katika kukidhi mahitaji ya wateja wetu tumepanda kutoka asilimia 40 kwa mwaka 2021/2022, hadi kufikia asilimia 80 kwa mwaka 2023/2024, jambo ambalo limepunguza uhaba wa bidhaa na malalamiko ya wateja” amesema Sungusia.

Pamoja na hali hiyo, amesema kuwa MSD imefanikiwa kuboresha jukumu lake la uhifadhi  kwa kuhakikisha inajenga maghala mapya kwenye kanda zake nchini, ambapo kwa sasa ujenzi huo unaendelea kwenye kanda za Dodoma, Mtwara katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.

“Na kuanzia na mwaka ujao wa Fedha 2024/25 tunatarajia kutaanza ujenzi wa maghala kwenye kanda za Kagera na Mwanza,” amesema

Katika hatua nyingine Sungusia amebainisha namna MSD ilivyoboresha usambazaji wa bidhaa za afya nchini kutoka mara nne hadi sita  kwa mwaka, ambapo zoezi hilo hufanyika kila baada ya miezi miwili huku maboresho hayo yakielezwa kuimarisha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

Naye Meneja wa MSD Kanda ya Kagera, Masatu Kalendero amewashukuru wadau hao kwa ushirikiano wao ambapo ameahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa huku akiwashi kuendelea kudumisha umoja na ushirikiano kama njia ya kuboresha afya kwa wananchi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here