*AVYOPOKEWA NA RAIS SAMIA MBELE YA WAJUMBE WA NEC, MWENYEWE ASEMA CHADEMA IMEPOTEZA MSINGI MBELE YA WATANZANIA, LEMA ATUMA UJUMBE WA KUUMIA KUONDOKA KWAKE, MDEE AMPA POLE
Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
NI suala la muda. Ndiyo unavyoweza kusemahasa baada ya mweyekiti wa zamani wa Kanda ya Nyasa kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa kuamua kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokewa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mchungaji Msigwa leo alichukua uamuzi huo Na kutambulishwa mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ambacho kilihudhuriwa na vigogo wa chama hicho tawala wa upande wa Bara na Visiwani.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu-Lumumba Jijini Dar es Salaam, Mchungaji Msigwa alimshukuru Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ambao wamempa mapokezi ya heshima Alasiri ya leo.
“Niseme kwa kifupi mambo mengine tutayaongea kwenye mikutano inayokuja, nilivyojinga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuna vitu ambavyo vilikuwa vimetuvutia baadhi yetu. Na ninaamini hata rafiki yangu Peneza (Upendo), anaweza kusema tulikuwa attracted na misingi ya chama.
“Chama kilituaminisha na kuna nyakati tuliona mambo hayo kwamba ni chama kinachosimamia misingi ya haki, uhuru, demokrasi na maendeleo ya watu kwa hiyo ni vitu ambavyo vilituatract (vilituvutia), uhuru wa mawazo ilikuwa ni misingi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo lakini kama mnayojua nimekuwa mwanachama mtiifu, mchapakazi na waminifu kwa chama change zaidi ya miaka 20 nimefaya kazi ya Chadema ndani ya chama.
“Lakini kwa kweli muda ulivyozidi kweda chama kile kimegeuka na kuwa Saccos ya mtu mmoja, ambaye yeye anaamua analolitaka liwe na linakuwa, tumekuwa wakosoaji wa kuikosoa Serikali ya CCM lakini tunakosoa yale ambayo sisi wenyewe hatuyafanyi, tumekuwa wazuri sana kukosoa kwamba Serikali kwaba haitekeleza ugatuaji mikoani hasa sera za majimbo, wakati sisi wenyewe ndani ya Chadema mambo haya hayafanyiki ni maneno tu ya majukwaani,” alisema Mchungaji Msigwa
Licha ya hali hiyo alisema wamekua wakosoaji ikiwamo kuhitaji Katiba Mpya ingawa katika hali ya kustaajabisha ndani ya Chadema hakuna anayeifuata Katiba ya chama hicho.
“Tumekuwa wakosoaji kwamba tunataka katiba mpya ni jambo jema kupata katia inayokidhi lakini katiba yetu wenyewe ndani ya chama(Chadema), hailindwi inavunjwa mtu mmoja anaweza kufanya anavyotaka kuamua yale ambayo yanaweza kufanyika.
“Tumekuwa tunakosoa utendaji wa baadhi ya watumishi wa umma kwamba wana maagizzo kutoka juu lakini hayohayo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo yanafanyika, sasa mimi kama mtu mzima mwenye uelewa na mwanasiasa mzoefu tunapata wapi uhalali wa kusimama kwenye majukwaa tukikosoa mfumo wa uchaguzi ndani ya CCM, ndani ya Serikali wakati mifumo ya uchaguzi ndani ya chama chetu ni mifumo ambayo mibaya zaidi kuliko ile tunayokosoa ndani ya Serikali,” alisema
HALI YA KISIASA NCHINI
Mchungaji Msigwa alikumbuka namna hali kisiasa ilivyoimarika kutokana na utashi wa Rais Samia tofauti na kipindi cha nyuma hatua ambayo ilisababisa kusitishwa kwa shughuli za mikutano ya kisiasa nchini.
“Tunakumbuka kwamba hata tulipotoka hali ya kisiasa ilikuwa ngumu, lakini alipoingia Mheshimiwa Rais Samia akaweka mazingira ya kufanya siasa na mikutano lakini leo tunakuta chopa inaruka unakuta mtu mmoja ameweka picha yake yeye anasahau kwamba hiki ni chama cha siasa ambapo kuna upana mkubwa ambao watu wanatakiwa kufanya.
“Kwa hiyo kwa kuwa tumepoteza misingi na hatuana uhalali wa kuikosoa CCM kwa wtu wengine wenye akili nimeona ni bora nishirikiane na Chama Cha Mapinduzi ambacho kimsingi huwezi kuchezea amani ambayo ipo mpaka sasa.
“…sisemi kwamba Chama Cha Mapinduzi ni malaika lakini mambo yanayofanyika ya utulivu na amani, uhuru wa mawazo ambao umepata mpaka sasa haya yahajazuka kumekuwa na Leadership (uongozi), unaoleweka ambao mimi binafsi nimekua attracted (nimevutiwa) kwamba kwa nini tusicollaborate (tusishirikiane) na Serikali iliyoko madarakani tukafanya kazi kwa pamoja badala ya kucompet (kushindana),” alisema Mchungaji Msigwa
HALI NDANI YA CHADEMA
Mchungaji Msigwa ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alisema ajenda ya chama chake hicho cha zamani imepotea mbele ya macho ya Watanzania.
“Ajenda ya ndani ya chama cha Chadema, kimepoteza mvuto na hawana ajenda na wala hoja na ndio maana mimi binafsi nimefurahi sana kuwa kwenye chama kikubwa hiki (CM), ambacho ninaamini kwa unyenyeku mkubwa weledi, uzoefu nilionao nikishirikiana na wakongwe alioko ndani ya Chama Cha Mapinduzi nitafanya nao kazi vizuri zaidi ili kuhakikisha tunalisukuma hili gurudumu la maendeleo.
“Ni matumaini yangu kama alivyosema Mheshimiwa Rais (Samia) kazi zipo nyingi za kufanya za kushirikiana pamoja kukijenga chama, nitashirikiana na wengine kuzunguka Tanzania nzima kuwaambia wananchi juu ya uongo, usanii wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambao viongozi wa juu wanaaminisha wananchi vile ambavyo hawako na kitu kibaya sana tunaongea mambo ambayo hatuyaishi.
“Tunaongea kuhusu demokrasi ndani ya chama hakuna demokrasi, tunaongea kuhusu ufisadi ndani ya chama kuna ufisadi, tunaongea kuhusu haki ndani ya chama hakuna haki tunapaswa tusimame tukiwa wasafi na mimi nafsi imenisuta kwamba siwezi kuendelea kuvumilia kuwadanganya wananchi kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni mbaya wakati sisi ni wabaya zaidi,” alisema Mchungaji Msigwa ambaye alitambulishwa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla kwenye mkutano huo.