Na MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wamemchagua Mhandisi Aivan Maganza kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Maganza anachukua nafasi hiyo ambayo ilikuwa wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Augustino Mrema kufariki dunia Agosti 21, 2022.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Rashid Amir, limtangaza Maganza kuwa mshindi baada ya kupata kura 33.huku wagombea wenzake wanne wakiangukia pua mara baada ya mwanga kishika nafasi ya pili kwa kupata kura 10 huku Stanley kura mbili na wagombea wawili wakipata kura sifuri.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, mwenyekiti huyo mpya wa TLP ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwa cha kisasa huku akituma salamu kwa vyama vingine kwamba vijipange.
“Wale ambao wako TLP kwa nia ya kukivuruga chama au kukikwamisha kuanzia sasa nawatangazia waondoke…nataka nibaki na watu wanaoweza kufanya kazi,” alisema Maganza.
Maganza pia amemteua Riziki Gaga kuwa Katibu Mkuu wa TLP baada ya Richard Lyimo kuasi chama na kuahidi kuunda upya sekretarieti ya chama hicho.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TLP, Dominata Rwechungura alisema kuwa wamepata wakati mgumu sana kuandaa uchaguzi huo mara baada ya kuandika barua mara kadhaa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ni mlezi wa vyama na baadae kufanikiwa kuitisha uchaguzi ambapo ameomba wajumbe kushikamana kujenga chama hicho ambacho Hayati Augustino Mrema amekipigania kwa jasho na damu .
Mwenyekiti huyo mpya wa TLP awali alikuwa Mwenyekiti wa Vijana taifa wa chama hicho.
Na kwa upande wake Katibu Mwenezi wa chama hicho, Geofray Stephen Laizar alisema ni wakati wa kushikamana kwa pamoja pasipo kuangali dini wala kabila.na kuonfoa makundi katika chama hicho .
Alisema baada ya kumpata mwenyekiti mpya chama kitaunda safu ya ushindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kisha kumsimamisha mgombea urais hapo mwakani 2025 .
Uchaguzi huo umefanyika nchini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi wakiwa na Silaha ambapo mwaka jana uchaguzi huo uliingia dosari baada ha aliyekua Katibu Mkuu wa TLP Richard Lyimo, kuarisha uchaguzi ghafla wakati wajumbe wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano tayari kwa uchaguzi.