Home KITAIFA MNDOLWA: NI AIBU KUIANGUSHA SERIKALI, CHAMA KWENYE MIRADI ISIYO  NA UBORA

MNDOLWA: NI AIBU KUIANGUSHA SERIKALI, CHAMA KWENYE MIRADI ISIYO  NA UBORA

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-DODOMA

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, amewataka wahandisi na watumishi wa Tume kuheshimu, kusimamia na kutekeleza miradi kwa viwango na ubora.

Amesema ni aibu kwa taasisi kuwa na miradi isiyokidhi viwango hivyo hatakuwa tayari kuona miradi hiyo inaiangusha serikali na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Mndolwa amesema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na menejiment, wasimamizi wa miradi, wahandisi wa mikoa na wahakiki ubora wa miradi na baadhi ya watumishi.

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa  ni muhimu kila mmoja kujua serikali inafanya kazi kubwa kuwezesha miradi hiyo kwa maslahi ya wananchi, hivyo ni muhimu usimamizi wake kuzingatia matokeo yenye ubora.

“Naomba kasimamieni miradi ni aibu kuwa na miradi isiyo na ubora, ni aibu kwenu na taasisi na tutaiangusha serikali na chama ambacho kinatutaka tutekeleze Ilani, mjue sitamuonea mtu lakini sitakuwa tayari kumvumilia yeyote asiyetekeleza wajibu wake, nitafanya mabadiliko mara kwa mara, lengo ni kuboresha utendaji na kuwa na ufanisi,” amesema

Kutokana na haki hiyo mesisitiza umuhimu wa watumishi hao kushirikiana na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala (DAHRAM), ambaye ndiye mratibu wa utekelezaji wa shughuli za mifumo ya serikali ndani ya Tume.

Aidha, amewakumbusha wahandisi wa umwagiliaji wa Tume kwa mikoa kuwa wasimamizi wa shughuli za utekelezaji wa majukumu ya tume ndani ya mikoa yao. Aliongeza kuwa wahandisi hao watapimwa kwa utekelezaji wa majukumu hayo.

Katika kuhakikisha ufanisi, Mndolwa amesisitiza watumishi wote kuheshimu sheria za utumishi, ikiwemo kufika kazini kwa wakati na kuvaa mavazi yenye hadhi.

Kuhusu mabadiliko ya uongozi, Mndolwa amesema ofisi yake inalazimika kufanya mabadiliko ndani ya idara na vitengo vya Tume ili kuongeza ufanisi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here