Home KITAIFA UHABA WA MAJI DAR WAMUONDOA BOSI DAWASA

UHABA WA MAJI DAR WAMUONDOA BOSI DAWASA

Google search engine
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua moja ya nyaraka katika ziara yake ya kushtukiza Jijini Dar es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiula Kingu

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA), Kiula Kingu, kukaa pembeni katika majukumu yake kwa muda, huku akimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji-DAWASA, Shaban Mkwanywe na kuanzia June 30, 2024.

Pamoja na hali hiyo pia ameiweka DAWASA chini ya uangalizi maalum wa Wizara ya Maji ili kuboresha utendaji wake kufuatia uzembe uliopelekea visima kukosa maji na kufanya wakazi wa Dar es salaam kukosa maji.

Aweso ametangaza uamuzi huo leo baada ya kufanya ziara ya kimkakati na ya kushtukiza katika Ofisi za DAWASA zilizopo Ubungo Dar es salaam ili kupata maelezo ya watendaji kuhusu wananchi kukosa maji baada ya kushindwa kuridhishwa na majibu aliamua kuzungukia matanki ya maji katika maeneo manne.

Maeneo hayo ambay aliyazungukia ikiwamo tanki la Ardhi UDSM na Kibamba huku akituma timu nyingine kwenda kukagua matanki ya Kigamboni ambapo imebainika matanki kadhaa hayana maji huku mengine yakiwa na maji kidogo ukilinganisha na mahitaji ya wananchi jambo ambalo watendaji wa DAWASA wameshindwa kueleza sababu iliyosababisha uhaba huo wa maji.

“Mwanzoni kulipokuwa kunakosekana maji tulikuwa tunasema shida ni vyanzo vya maji vimekauka hakuna maji, TANESCO umeme hamna lakini leo vyanzo vyote vina maji, umeme upo, niambieni kwanini hatuna maji kwenye matanki?, kwanini wananchi wanateseka, wanalalamika wanapiga kelele kwa serikali, niiombe bodi kama CEO DAWASA hajaenda likizo kidogo akakae likizo kwanza atuachie nafasi yetu tutaisimamia wenyewe,” amesema Waziri Aweso

Ziara hiyo ya Aweso imekuja baada ya ziara ya Katibu Mkuu wa Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri aliyoifanya kwa siku mbili kujionea utendaji kazi wa DAWASA na hali ya upatikanaji wa maji Dar es Salaam ambapo amebaini uzembe aliouwasilisha kwa Waziri ikiwemo miundombinu ya maji kuwa chakavu, maji kupotea bila usimamizi, Watendaji wa DAWASA wa ngazi za chini kutopewa stahiki zao muhimu na kupelekea kufanya kazi bila hamasa nzuri na hata kupelekea kuwajibu vibaya wateja wa maji.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here