Home KITAIFA MSD ILIVYOTAFSIRI DHANA YA  KUJITEGEMEA KWA VIFAA TIBA

MSD ILIVYOTAFSIRI DHANA YA  KUJITEGEMEA KWA VIFAA TIBA

Google search engine

*GLOVES PEA MILIONI 86.4 KUZALISHWA KIWANDA CHA IDOFI, MAKAMBAKO

Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Gloves kinachomilikiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe, Mhandisi Shiwa Mushi (kushoto) akitoa maelezo ya uzalishaji kwa Wahariri waliotebelea kiwanda hicho

Na MWANDISHI WETU

– NJOMBE

KAZI Inaendelea. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Bohari ya Dawa (MSD) kuitafsiri kwa vitendo kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kiwanda cha Mipira ya Mikono (Gloves) kilichopo Idofi Halmashauri ya Makambano mkoani Njombe kuanza rasmi kazi.

Kutokana na hali hiyo kiwanda hicho kwa sasa kimeanza uzalishaji wa bidhaa tiba hizo milioni mbili hadi sasa ukiwa mkakati wa kukuza uchumi na kuimarisha sekta ya afya nchini.

Akizungumza na timu ya wahariri wa vyombo vya habari iliyotembelea kiwandani hapo leo Julai 2, 2024, Kaimu Meneja wa Kiwanda Glovu Idofi kinachomilikiwa na Bohari ya Dawa (MSD) Mhandisi Shiwa Mushi, amesema kuwa kiwanda hicho kilijengwa Oktoba 4, 2020 na ujenzi wake ulitokana na changamoto ya iliyoibuka mwaka 2019 ya Ugonjwa wa Korona (Uviko-19).

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa miongoni mwa changamoto walizozipata MSD na nchi kwa ujumla ni uingizaji wa vifaa tiba kutokana na vizuizi na uagizaji wa dawa ilikuwa changamoto kubwa.

Amesema hali hiyo iliichohea MSD na taifa kwa ujumla kuona haja ya kuanzisha viwanda vyake hasa kutokana na hali hiyo ambayo inatajwa kuwa somo na kuamua kuja na mkakati wa kuwa na kiwanda cha glaves.

“Na ukiweza kuvaa glave utaweza kuwahudumia wagonjwa hata kama ni wa Korona kwa usalama zaidi kwa hiyo tukaanza na Kiwanda cha gloves.

“Kiwanda hiki kimejengwa hapa Idofi Makambako na hili eneo lote lina ukubwa wa ekari 38 na MSD inalimiki kisheria na ililitwaa kutoka kwa wananchi wa Idofi na tumewalipa na sasa eneo hili lina hati.

“Hili eneo kuna majengo mengi ambayo yanakwenda kutoa picha ya Kiwanda cha Gloves na kiwanda chetu na jengo hili la kiwanda lina urefu wa mita 130, upana mita 124 kwa maana kwamba ukiangalia ni mita za mraba 3,120. Awali bidhaa hizi tulikuwa tukiagiza nje ya nchi lakini kutokana kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wa MSD sasa tunafanya hapa nyumbani Tanzania, hii ni fahari kwetu kama taifa na Watanzania kwa ujumla,” amesema Mhandisi Mushi

Amesema katika majengo hayo lipo jengo la malighafi kwa ajili ya uzalishaji na majengo mawili mengine wamepanga yatakuwa kituo cha Kiwanda cha Gloves huku wakiwa na mkakati madhubuti wa biashara wataongeza majengo mengine.

“Kwa upande wa kulia kwenye michoro yetu kuna majengo ambayo kwa sasa yapo kwa ajili ya uhifadhi wa bidhaa. Na mikakati ya kiwanda kuzalisha aina mbili Gloves Surgical (zinazotumika kuvaa kwenye upasuaji) na Examination Glove (Glovu zinazovaliwa wakati wa uchunguzi wa awali) na hii unaweza labda umekwenda hospitali unaumwa daktari huzivaa kwa ajili ya kukuangalia,” amesema

MKAKATI WA KIWANDA

Amesema kiwanda hicho kimebakisha sehemu mbili katika mkakati wa uzalishaji ikiwamo kwenda kuzalisha pisi 20,000 ambazo ni sawa na pea 10,000 na hiyo ikiwa kitazalisha katika hali yake ya kawaida.

“Na kiwanda hiki ukifanya mahesabu kitaalamu inaonyesha kwamba kwa mwaka kitazalisha jumla ya gloves pea milioni 86.4, ambazo ni sawa na asilimia 86.34 ya mahitaji ya nchi. Kwa hali hii unaweza kuona kiwanda hiki ni kikubwa kwa kiasi gani na sasa tumebaki na uzalishaji wa Examinationa Glaves, ambapo katika kuzalisha kunahitajika malighafi.

“…malighafi mama ambayo inatumika zaidi ni utomvu ambao hutokana na mti wa zao la mpira, ambapo kinachofanyika huvunwa ule uteute kama maziwa na unapopatikana huchanganywa na baadhi ya kemikali ili kuweza kufikia viwango vya kuzalisha. Utomvu unapopatikana unakuwa kwenye utayari na hutumika kama malighafi kwenye uzalishaji, katika kuzalisha pindi tutakapoingia kiwandani tutaona zile hatua za mtambo ambao una urefu wa mita 100 na una line mbili (mistari miwili),” amesema Mhandisi Mushi

Kaimu Meneja huyo amesema kuwa katika uzalishaji kuna hatua mbalimbali kwa sababu bidhaa za afya zinahitaji umakini na usafi wa hali ya juu.

Alitaja hatua hizo ikiwamo ile ya kwanza ya kusafisha ikiwamo sampuli za mikono ambazo husafishwa ambapo huingizwa kwenye maji ikiwamo Acid (kemikali) ambazo huandaa mikono kwa ajili ya kupokea malighafi.

“Baada ya hapo zinaingizwa kwenye malighafi yenyewe ya mikono ambapo kuna taratibu kadhaa hufanyika ikiwamo kuzikausha. Na kisha zinakwenda kwenye kemilika mingine ya rich process kuweza kuondoa madhara na hutumika saa moja kwenye mchakato wa ukaushaji wa mipira ya mikono.

“Ukishamilika hatua inatofuatiwa ni uvuaji kwa upande wa Surgical zina mtambo wa uvuaji kwa sababu surgical ni proces (mchakato). Baada ya zikishavuliwa zinapelekwa maabara kama unavyofahamu bidhaa za afya zinahitaji umakini sana salama kwa sababu zinatumika katika mwili wa binadamu,” amesema

UBORA WA BIDHAA

Kaimu Meneja huyo, amesema kuwa baada ya hatua hiyo bidhaa hizo huingizwa maabara kwa sababu ya kuangalia ubora na kuhakikiwa, zinakaushwa na kisha zinaingizwa sehemu nyingine ya pili Clean room (chumba kisafi), hiyo maana yake ni sehemu ambayo hakuna vijidudu kule control (udhibiti) wake ni mkubwa.

“Kwa hiyo bidhaa inaingia kule inajaribiwa baada ya kujaribiwa huwekwa kwenye vifungashio (Parckage Material) na kisha inapelekwa sehemu maalum kama sehemu ya kuhifadhia ambao huitwa Karantini ambapo watalaam wanakagua kama mzigo upo vizuri.

“Na baada ya hapo huchukuliwa kwa ajili ya kuingia sokoni kwa kifupi mpaka tunatoa glave kama nilivyosema Batch moja ya uzalishaji inahitaji karibia saa moja,” amesema

UKAGUZI WA MAMLAKA

Mhandisi Mushi, ameweka wazi kwamba kiwanda hicho kinafanya hivyo tangu kilipoanza uzalishaji Februari 12, mwaka huu na kilianza baada ya kupata vibali vyote vya mamlaka za udhibuti ikiwamo TMDA ambao walitoa kibali cha ubora.

“Walikuja hapa kukagua mara nyingi sana ikiwamo kufanya marekebisho mbalimbali na mwisho walitupa kibali mnamo mwezi wa kwanza mwishoni ikiwamo Certificate of Compliance na pia tukapewa na kibali cha usajili wa bidhaa ambacho kilisajili na TMDA.

“Lakini pia tukapewa vibali na Jeshi la Zimamoto na Ukoaji ambao walikagua na wakatoa cheti pia tulikaguliwa na GSLA ambao waliangalia matumizi na udhibiti wa kemikali kama tupo sawa,” amesea Mhandisi Mushi

HALI ILIVYO SASA

Amesema kuwa baada ya kupata vibali hivyo kutoka kwenye taasisi hizo, kazi ya uzalishaji ilianza Februari hivyo mpaka sasa wanaendelea na kazi hiyo ikiwamo kuzalisha bidhaa hiyo.

“Tunaendelea na uzalishaji na tumeshazalisha takribani Gloves pea milioni mbili ambazo ni sawa na pisi milioni nne mpaka sasa zimeshazalishwa, zoezi linaloendelea sasa hivi ndani ni kufungasha kwa wiki tunazalisha siku tatu ambazo ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa sababu hutumia malighafi ya utomvu na kemikali.

“Kwa hiyo ziku hizo tatu kuna watalaam wa maabara, ubora a baada ya siku tatu hujiridhisha kwamba inafaa kuzalishwa. Siku ya Jumatatu huwa tunafanya usafi wa mtambo na Jumanne huwa tunafanya matengenezo madogo madogo,” amesema Meneja huyo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here