Na MWANDISHI WETU
RAIS wa Filamu Korea Kusini Yang Jongkon amesema Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya kwanza Africa kufanya movie na nchi hiyo huku akiahidi kuja nchini akiwa kuonana na waigizaj wa filamu.
Akizungumza na baada ya waigizaji katika mji unaoongoza kwa filamu duniani ujulikanao kama Busan amesema Rais huyo wa filamu Korea kusini YANG Jongkon amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kuunganisha soko la filamu la Tanzania na Korea.
“Hivyo basi nami sina budi kueleza kuwa Tanzania ndio nchi ya kwanza tutakayoshirikiana nayo tutakapoingia Afrika. Kwa sasa tunamalizia kuimarisha bara la Asia kwenye tasnia hii ya filamu,” amesema.
Waigizaji hao ambao wapo katika ziara ya kujifunza makubwa zaidi katika soko la filamu nchini Korea kusini wameahidiwa na wameahidiwa makubwa na Rais Jongkon.
Rais Yang Jongkon ameahidi kuja Tanzania kuonana na wasanii wa Tanzania akiongozana na baadhi ya watengeneza filamu wa Korea.
Wasanii kutoka Tanzania wamefanikiwa kutembelea Studio kubwa za Busan na kuona jinsi filamu za kikorea ambazo zimetokea kupendwa sana na watanzania zinavyotengenezwa.
Filamu hizo maarufu zinazotambulika kama Kdrama(Korean drama) zimetokea kuiteka dunia na kuiweka Korea juu kabisa katika masoko ya filamu kimataifa.
Wakati Rais YANG Jongkon akizungumza hayo mjini Busan aliendelea kwa kukazia kuwa atahakikisha anaendelea kuudumisha na kuimarisha uhusiano mzuri sana uliopo kati ya Tanzania na Korea Kusini.
Ameshukuru sana kwa zawadi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ilikabidhiwa na kiongozi wa msafara huo wa wasanii Steve Nyerere.