Home KITAIFA NIRC YAKABIDHI MRADI WA BILIONI 5.2/-  KWA MKANDARASI MKOANI NJOMBE

NIRC YAKABIDHI MRADI WA BILIONI 5.2/-  KWA MKANDARASI MKOANI NJOMBE

Google search engine

Na MWANDISHI WETU

-NJOMBE

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), imekabidhi kazi ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji katika Kijiji cha Itipingi mkoani Njombe kwa mkandarasi wenye thamani ya Shilingi bilioni 5.2.

Awali mradi huo ulijengwa kwa gharama ya Shilingi milioni 400, ambapo kutokana na maboresho yaliofanywana NIRC sasa baada ya kukailika uakuwa mkubwa zaidi na kuweza kuhudumia wakulima wengi.

Akizungumza leo Julia 10, 2024 baada ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka, ameiagiza halmashauri ya wilaya ya hiyo kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima wa na kutumia mradi huo ipasavyo.

Kutokana na hali hiyo amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira ya mradi ikiwemo kupima mashamba na viwanja pamoja na kuandaa teknolojia za kisasa za kilimo kama njia ya kuandaa masoko ya uhakika kwa mazao yatakayozalishwa kwenye eneo hilo la mradi.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Itipingi, Mkuu wa Mkoa Mtaka, amewaasa wananchi kwa kuhakikisha wanautunza mradi huo kwa kuacha kupeleka mifugo katika eneo hilo.

“Ninachowaomba wananchi akikisheni tunautunza mradi huu muhimu kwa ajili ya kuimaisha sekta ya kilimo atika mkoa wetu, vijana nyie ndio walinzi wa kwanza msiibe vifaakatika eeo hilo na badala yake ulindeni,” amesema Mtaka

Naye Mhandisi wa Tume Mkoa wa Njombe, Machage Mwema, amesema kuwa baada ya usanifu wa pili,mkataba wa ujenzi huo  ulisainiwa baina ya serikali na mkandarasi kutoka kampuni ya Sihotech Engeneering Company Ltd na AMJ Global Multi Contractor  Co Ltd,  June 24, mwaka huu Jijini Dodoma.

Akizungumzia shughuli ambazo mkandarasi huyo atafanya kwa kipindi cha miezi 14 ya ujenzi wa mradi huo kuwa ni pamoja na kukarabati miundombinu  iliyojengwa kwenye ujenzi wa awali, kundeleza na kujenga mfereji mkuu, kujenga mifereji ya umwagiliaji, kujenga barabara za kuzunguka mashamba, ujenzi wa madaraja.

Pia atajenga vivusha maji, barabara kutoka eneo la mradi mpaka kijijini kwa ajili ya kusafirisha pembejeo na mazao pamoja na kujenga ofisi ya mhandisi wa umwagiliaji.

“Kutokana na ukubwa wa mradi Serikali itanunua gari moja kwa ajili ya kuhudumia mradi na kwamba kazi ya ujenzi huo inaanza siku 14 baada ya mkandarasi kukabidhiwa kazi na kuwa mradi huo unalenga kuwahudumia wakulima 417.

“Hata hivyo idadi inaongezeka kutoka wakulima 77 waliotarajiwa katika mradi wa awali. Wanufaika wa mradi watatoka vijiji vya Itipingi, Kiumba na Malombwe, Halmashauri za Makambako na Njombe,” amesema

Kwa upande wa wananchi wa Kijiji cha Itipingi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Igongolo, Isaya Myamba, aliishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kujenga mradi huo kwa mara ya pili.

Amesema kiu ya wakulima wa eneo hilo ni kuhakikisha wanakuwa na mazingira mazuri ya kilimo ili kuweza kustawisha kilimo cha mbogamboga kwa wingi kama njia ya kuyafikia masoko makubwa ya kilimo.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here