Home KITAIFA TANZANIA YAELEZA UMUHIMU MATUMIZI RASILIMALI MADINI YA KIMKAKATI

TANZANIA YAELEZA UMUHIMU MATUMIZI RASILIMALI MADINI YA KIMKAKATI

Google search engine
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo akichangia mada kuhusu kuhamasisha utekekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu 2030 katika Mkutano wa viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Pili wa Ngazi ya Juu wa Jukwaa la Hatua za Dunia kwa Maendeleo ya Pamoja Baijing, China.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo,akiwa na ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa viongozi mbalimbali wa Pili wa Ngazi ya Juu wa Jukwaa la Hatua za Dunia kwa Maendeleo ya pamoja Beijing nchini China, engine ni Balozi wa Tanzania nchini hapa Khamis Mussa Omari (wapili kushoto), Katibu wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru (wapili kulia), Ellykedo Ngonyani na George Mukono.
Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar akiwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru,  wakifuatilia mjadala katika Mkutano wa Pili wa Ngazi ya Juu wa Jukwaa la Hatua za Dunia kwa Maendeleo ya Pamoja Baijing, China

Na MWANDISHI MAALUM

TANZANIA  itatumia rasilimali ya madini ya kimkati kukuza uchumi wa viwanda na kutoa mchango wake kwa Dunia katika kutimiza malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo alipohihitimisha ziara yake ya kikazi nchini China alikohudhuria Mkutano wa Kimataifa ulioangazia namna ya kuharakisha malengo endelevu ya Dunia 2030 (SDGs).

Prof. Kitla, alisema kuwa mkutano huo ulibaini kuwepo kwa changamoto zinazoyakabili mataifa mengi duniani, umasikini na mabadiliko ya tabianchi yakiwa kitovu cha mjadala katika vikao mbalimbali vya mkutano huo.

“Tumeona katika mijadala kwamba, ili kuondoa umasikini tunahitaji uwekezaji katika ujenzi wa Miundombinu na teknolojia ya mawasiliano,” alisema Prof. Mkumbo.

Pamoja na hali hiyo Profesa Kitila, alisema kuwa Tanzania ina nafasi ya kutoa mchango wake wa kutatua changamoto hizo kwa dunia hasa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Kuelekea 2030 Dunia itabadilisha nishati, sisi Tanzania tuna madini yanayotumika kutengeneza betri za magari, hivyo tumetumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kuzalisha betri.

“Wakifanya hivyo, tutaisaidia Dunia kutumia nishati safi, wao watakuwa wanatusaidia kupunguza umasikini, kwani hakuna nchi imeendelea bila kujenga viwanda,” alisema Prof. Kitila

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini China, Khamis Mussa Omar aliweka wazi kuwa uhusiano wa China na Tanzania umeimarika sana katika sekta mbalimbali na sasa umetimiza miaka 60 na kuingia katika hatua mpya.

“Tangu tumeanzisha uhusiano na China miaka 60 iliyopita, tumekuwa na ushirikiano muhimu katika sekta za ujenzi wa miradi inayonufaisha jamii kama, kilimo, viwanda na miundombinu,” alisema Balozi Omar.

Mkutano huo umekuwa wenye manufaa makubwa kwa Tanzania kwa kuwa umeangazia changamoto ambazo dunia inapitia katika utekelezaji wa Mipango yake inayosimawiwa na Mkakati wa Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs).

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru, alisema kuwa mijadala iliyoendelea katika Mkutano huo imekuwa muhimu kwa Tanzania kuelekea katika uandishi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni ya kuzingatia katika mipango yetu na uandishi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, bila kufanya hivyo, tutajikuta tupo katika mtanziko kama Dunia ilivyo leo kuhusu SDGs, Dira yetu isisahu kuwekeza kwenye elimu ya watu wetu ili watumia ujuzi na maarifa kuleta maendeleo.

“…vile vile, tumeona mijadala umesisitiza kuwa watu wenye Afya ndiyo ufunguo wa uzalishaji, uwekezaji kwenye Afya za watu wetu ni muhimu,” alisema Mafuru.

Mkutano huo pia umekuwa miongoni mwa vielelezo vya uhusiano wa kihistoria baina ya Tanzania na China kwa kuwa mbali na Waziri Prof Kitila kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la China (CDICA), ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi walioalikwa kukutana na Naibu Waziri Mkuu Mkuu wa nchi hiyo, Liu Guozhong.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here