Na MWANDISHI WETU
-RUKWA
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema sababu ya nusu ya mradi wa vihenge mkoani Rukwa kuchelewa kukamilika akitaja mgogoro uliotokea na mkandarasi, japokuwa tayari wametatua changamoto hizo.
Waziri Bashe amesema hayo Julai 16, 2024 wakati akizungumzia ujenzi wa vihenge hivyo ambavyo vimezinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“TBA (Wakala wa Majengo Tanzania) wamesimamia mradi huu tangu 2019/2020 na wamekamilisha nusu ya mradi lakini, nusu haijakamilika kwasababu kuliingia mgogoro kidogo na mkandarasi…tumewaagiza walimalize hilo ili tumalizie vihenge vingine.
“Rais ametoa maelekezo ya kuongeza vihenge na tumeshakubaliana na Mkurugenzi Mtendaji wa NFRA (Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula) kwa ajili ya kuongeza vingine,”amesema Waziri Bashe.
Waziri Bashe amepongeza usimamizi uliofanywa na TBA hadi kukamilika kwa mradi huo awamu ya kwanza kwa asilimia 100.