Home KITAIFA DK. KALUMANGA: USHIRIKISHWAJI SEKTA BINAFSI HUSAIDIA UHIFADHI NCHINI

DK. KALUMANGA: USHIRIKISHWAJI SEKTA BINAFSI HUSAIDIA UHIFADHI NCHINI

Google search engine
Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Waandshi wa Habari za Mazingira Taznzania (JET) Dk. Ellen Ottaru, leo mjini Bagamoyo

Na MWANDISHI WETU

-BAGAMOYO

SEKTA binafsi ni ile sehemu ya uchumi ambayo huendeshwa kwa faida binafsi na haidhibitiwi na serikali.

Kutokana na hali hiyo imebainika kuwa sekta ya wanyamapori inaweza kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ikiwa sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu katika shughuli za uhifadhi endelevu.

Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga

Akizungumza katika Mafunzo kwa Wahariri wa vyombo vya habari, yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Meneja wa Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi, mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga, amesema kuwa hatua hiyo imesaidia kuimarishwa kwa shughuli za utalii na utunzaji wa shoroba za wanyamapori nchini.

Amesema Wanyamapori wanaopatikana katika hifadhi za Taifa na maeneo mengine tengufu wamekuwa wakitumika katika shughuli za utalii na uwindaji na hivyo kuipatia nchi mapato ambayo yanatumika katika kuboresha huduma za kijamii.

“Ikiwa sekta binafsi itashirikishwa kikamilifu  inaweza kuendelea kuwa na mchango katika pato la Taifa, ikiwa wadau wote ikiwemo sekta binafsi watashiriki katika uhifadhi endelevu wa wanyamapori ambao kwa sasa unatishiwa na mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la watu katika maeneo ya uhifadhi na ukosefu wa rasilimali watu na fedha,” amesema Dk. Kalumanga

Pamoja na hali hiyo amesema kuwa ipo haja ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kukabiliana na changamoto zinazokwamisha shoroba za wanyamapori na makazi kama mkakati wa kulinda na kuhifadhi viumbe hai nchini.

Amesema hatua ya kujenga uwezo wa kitaasisi wa wadau wa umma na sekta binafsi, pia utakuza ushiriki wa sekta binafsi katika uhifadhi wa viumbe hai na usimamizi wa rasilimali za asili.

“Hatua hiii itasaidia sana kuboresha sera, kanuni, na mazingira ya kuwezesha uhifadhi wa viumbe hai na usimamizi wa rasilimali za asili. Lakini hili huonekana manufaa yake ikiwa sekta binafsi itashirkishwa.

“Lakini yapo manufaa kadhaa ambayo sekta binafsi imeweza kushirikishwa na kuingiza fedha za kigeni zaidi ya dola za Marekani zaidi ya milioni 2. lakini pia wanasaidia katika kutoa utaalamu katika usimamizi wa Rasilimali za Asili, ikiwamo  mbinu mpya katika Kupambana na Ujangili.

“Pia sekta binafsi hujua mifumo ya masoko ya bidhaa kama shanga na nyinginezo na si hilo tu pia husaidia miradi ya jamii kupitia Ushirikiano wa Umma na Binafsi (PPP),” amasema Dk. Kalumanga

Pamoja na hali hiyo amesema kuwa hatua hiyo husaidia kupata matokeo kadhaa kwa jamii ikiwamo kutoa ulinzi wenye ufanisi wa makazi na aina ya wanyama katika shoroba ikiwamo eneo la Kwakuchinja wilayani Babati mkoani Manyara.

“Pia kwa kuirikisha sekta binafsi husaidia ufuatiliaji wa aina ,kuongoza usimamizi wenye ufanisi hasa kwenye mikoa yenye changamoto ya Wanyamapori, shoroba za anyamapori (CWT/HWC). Ikiwamo kukuza ufugaji wa ng’ombe kwa njia endelevu katika shoroba ya Kwakuchinja ikiwamo kutoa mafunzo kwa wanachi kufuga kisasa,” amesema

Baadhi ya Wahariri walioshiriki mafunzo hayo
Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here