Google search engine
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula akiwa na Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka (CCM) aktika mkutano wa wananchi wilayana hapa

Na ANANGISYE MWATEBA

-LINDI

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amekemea tabia ya baadhi ya watumishi wa umma kuchelewa kufikisha Wizarani kwa wakati taarifa za tathmini ya athari wanazopata wananchi kutoka kwa wanyama wakali na waharibifu.

Amesema ucheleweshwaji huo wa taarifa unasababisha wananchi kuchelewa kupata kifuta jasho na machozi kwa wakati.

Hayo ameyasema kwa nyakati tofauti akiwa kwenye ziara ya kikazi katika wilaya za Ruangwa na Liwale mkoani Lindi kwa lengo la kukutana na wananchi na kuelezea jitahada zinazifanywa na serikali kudhibiti changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo, taarifa za tathimini zinapaswa kufikishwa Wizarani ndani ya siku saba baada ya majanga kutokea; lakini kwa sasa madai huchukua muda mrefu kufikishwa wizarani na hivyo kufanya mchakato mzima kuchukua muda mrefu kushughulikiwa.

Akiwa wilayani Liwale, alizitaka serikali za vijiji wilayani humo kudhibiti ufugaji holela kufanyika kwenye maeneo yao ya vijiji, na kushauri kuwa wafugaji wenye makundi makubwa ya ng’ombe waelekezwe kwenda kwenye maeneo maalum yaliyotengwa na halmadhauri kwa ajili ya ufugaji.

“Tusiwaache wafugaji waingize mifugo yao kwenye mapori na hifadhi kufanya uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira wanayoishi wanyamapori kwani kwa kufanya hivyo kunawafanya tembo kuja kutafuta maji na chakula  kwenye makazi ya watu,” amesema

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Hassan Ngoma akizungumza katika mkutano wa wananci ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Sustan Kitandula

Aidha Kitandula aliongeza kuwa serikali inatambua changamoto iliyopo ya wanyama wakali na waharibifu na kwamba serikali itafanya kila linalowezekana kudhibiti hali hiyo, na alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wananchi wanaokabiliwa na changamoto hiyo.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma alimshukuru Naibu Waziri ameahidi  kuchukua hatua kwa watendaji ambao hawatimizi wajibu wao wa kufanya tathimini ya majanga ya wanyama wakali na waharibifu kwa haraka.

Pia amemuahidi kuwasimamia kwa ukaribu askari wa uhifadhi ambao wataletwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Goodluck Mlinga na Mbunge wa Liwale, Zubari Kuchauka waliishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuitengea wilaya hiyo mabomu baridi 700 kwaajili ya kutumika kudhibiti tembo wilayani Liwale.

Aidha waliiomba wizara kuona uwezekano wa kuongeza askari wa uhifadhi katika wilaya hiyo ambayo inaeneo kubwa ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya eneo lote la mkoa wa Lindi.

Google search engine

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here